Wakati wa kumuomboleza mwanaharakati aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi
afrika Kusini Winnie Mandela, siku moja, kundi la waumini walioonekana kulewa walizua kionja.
Walikuwa wakilia na kuimba "Mama, Mama". Walijitetea kwamba nao pia walikuwa na haki ya kumuomboleza mtu waliyemuenzi sana.
Kiongozi wao alikuwa amevalia mavazi ya kidini.
Hakuwa mwingine ila Papa Makiti kiongozi wa kanisa jipya nchini Afrika Kusini ambalo limekuwa likiwashangaza wengi.
Kanisa hilo linalofahamika kwa jina Gobola (yaani nipe Ulevi ninywe kidogo kwa Lugha ya Kitswana, moja ya lugha rasmi nchini humo) lina mwaka mmoja hivi tangu lianzishwe.
Mwasisi wa kanisa hilo ni Tsietsi D Makiti, 53, ambaye kwa sasa anajiita Papa Makiti. Hujieleza kama papa wa kwanza mweusi kutoka bara la Afrika.
Alilianzisha kanisa hilo katika baa moja, na kanisa hilo hufanya ibada zake katika baa na vilabu.
No comments:
Post a Comment